Mwanamke Jithamini ยท @dr_nkindwa_tz

Posted 1 month ago
2.56K followers
450 views
3 likes
0 comments
0 shares

๐—จ๐—ž๐—˜ ๐— ๐—ž๐—”๐—ฉ๐—จ: ๐—ฆ๐—”๐—•๐—”๐—•๐—จ, ๐——๐—”๐—Ÿ๐—œ๐—Ÿ๐—œ ๐—ก๐—” ๐— ๐—”๐——๐—›๐—”๐—ฅ๐—” ๐—ž๐—ช๐—˜๐—ก๐—ฌ๐—˜ ๐— ๐—”๐—œ๐—ฆ๐—›๐—” ๐—ฌ๐—” ๐—ก๐——๐—ข๐—” Uke kuwa mkavu ni changamoto inayoweza kumuathiri mwanamke kimwili, kihisia na hata kwenye mahusiano ya ndoa. Uke unapokuwa na ute wa asili wa kutosha, husaidia kupunguza msuguano wakati wa tendo la ndoa. Ute unapopungua, msuguano huongezeka na tendo linaweza kuwa la maumivu. ๐Ÿ”น ๐—ฆ๐—”๐—•๐—”๐—•๐—จ ๐—ž๐—จ๐—จ ๐—ญ๐—” ๐—จ๐—ž๐—˜ ๐—ž๐—จ๐—ช๐—” ๐— ๐—ž๐—”๐—ฉ๐—จ 1. Kutokuwa na msisimko wa kutosha Mwanamke anapokuwa hajapata muda wa kutosha wa msisimko kabla ya tendo, ute wa asili unaweza kuwa mchache. 2. Mabadiliko ya homoni Kupungua kwa estrogen, hasa wakati wa kunyonyesha, baada ya kujifungua au kuelekea ukomo wa hedhi, kunaweza kusababisha ukavu. 3. Msongo wa mawazo na hofu Stress, uchovu, hofu na matatizo ya kihisia yanaweza kupunguza msisimko na ute wa asili. 4. Baadhi ya dawa Dawa fulani zinaweza kuwa na ukavu wa uke kama mojawapo ya madhara yake. 5. Kutumia sabuni au kemikali sehemu za siri Sabuni kali, dawa za kusafisha uke na kuosha uke ndani (douching) kunaweza kuvuruga mazingira ya kawaida ya uke. 6. Kuugua magonjwa ya uzazi kama uti, fangas, miwasho, pid nk mara kwa mara. ๐ŸŒธ ๐— ๐—”๐——๐—›๐—”๐—ฅ๐—” ๐—ฌ๐—” ๐—จ๐—ž๐—˜ ๐— ๐—ž๐—”๐—ฉ๐—จ ๐—ช๐—”๐—ž๐—”๐—ง๐—œ ๐—ช๐—” ๐—ง๐—˜๐—ก๐——๐—ข ๐Ÿ”ธ Maumivu wakati wa tendo Msuguano unapoongezeka, mwanamke anaweza kuhisi maumivu, kuwaka au kuungua wakati wa tendo. ๐Ÿ”ธ Michubuko na majeraha madogo Uke unapokuwa mkavu sana, msuguano unaweza kusababisha michubuko midogo kwenye ngozi ya uke. ๐Ÿ”ธ Kutokwa na damu baada ya tendo Michubuko au majeraha madogo kutokana na msuguano yanaweza kusababisha damu kidogo wakati au baada ya tendo. Kutokwa damu mara kwa mara baada ya tendo kunahitaji uchunguzi wa kitabibu, kwa sababu kuna sababu nyingine pia zinazoweza kusababisha hali hiyo. ๐Ÿ”ธ Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa Mwanamke akijua kwamba tendo litasababisha maumivu, anaweza kuanza kulihofia na hatimaye kupoteza hamu ya tendo. ๐Ÿ”ธ Kupungua kwa hisia wakati wa tendo Ukavu, maumivu na kutokuwa na msisimko wa kutosha vinaweza kufanya tendo lisilete hisia nzuri kama zamani. ๐Ÿ”ธ Kuathiri uhusiano wa ndoa Maumivu yanapojirudia, mwanamke anaweza kuanza kukwepa tendo. Ikiwa mwenzi haelewi sababu, hali hii inaweza kuleta kutokuelewana, malalamiko na migogoro katika ndoa. โค๏ธ Jambo muhimu la kuelewa Uke mkavu si jambo la kuonewa aibu wala kuvumilia maumivu kimya kimya. Tatizo likigundulika chanzo chake, kuna njia salama za kusaidia kulitatua. Mwanamke anayepata ukavu unaoendelea, maumivu wakati wa tendo, kuwasha, kuungua au kutokwa damu baada ya tendo anashauriwa kuonana na mtaalamu wa afya kwa uchunguzi badala ya kutumia vitu kama limao, chumvi, sabuni au dawa zisizothibitishwa ndani ya uke. #mwanamkejithamini #afyayauzazinaushauri #viral #friday #inshallah