Dr Jonem | Afya ya Uzazi · @dr.jonem

Posted 1 day ago
5.09K followers
74 views
2 likes
0 comments
0 shares

PID INAWEZAJE KUSABABISHA UTASA? PID ni maambukizi ya viungo vya uzazi vya mwanamke. Yakichelewa kutibiwa, yanaweza kusababisha uvimbe na makovu kwenye mirija ya uzazi. ✅ Mirija inaweza kuziba au kupungua uwazi. ✅ Mbegu za mwanaume zinaweza kushindwa kufika kwenye yai. ✅ Yai lililorutubishwa linaweza kushindwa kufika vizuri kwenye kizazi. ✅ Hii inaweza kusababisha ugumu wa kupata ujauzito au kuongeza hatari ya mimba kutunga nje ya kizazi. ⚠️ PID ikitibiwa mapema, hupunguza hatari ya madhara ya muda mrefu. 📞 0769828864 #PID #Utasa #KukosaMimba #AfyaYaUzazi #DrJonem