Posted 2 months ago
2.56K followers
408 views
10 likes
0 comments
0 shares
๐๐จ๐๐๐ฆ๐ ๐๐จ๐จ๐ก๐๐จ๐ ๐๐จ ๐ ๐๐ช๐๐ฆ๐๐ข ๐ช๐๐๐๐ง๐ ๐ช๐ ๐๐จ๐๐ข๐๐ข๐ ๐๐ช๐ ๐ ๐ช๐๐ก๐๐ ๐๐ ๐ฆ๐ ๐๐๐ ๐๐ข ๐๐ ๐๐จ๐ฃ๐จ๐จ๐ญ๐ Je, umewahi kuhisi kuungua, kuwashwa au maumivu unapokojoa? Wanawake wengi hupuuza dalili hizi wakidhani zitaisha zenyewe. Hata hivyo, hali hii inaweza kuwa ishara ya maambukizi ya njia ya mkojo (UTI). Ikiwa maambukizi haya yanajirudia mara kwa mara au hayaponi vizuri, yanaweza kuwa UTI sugu, ambayo inahitaji uchunguzi na matibabu ya mapema ili kuepuka madhara. ๐น ๐๐๐๐๐๐ ๐ญ๐ ๐จ๐ง๐ ๐๐ช๐ ๐ ๐ช๐๐ก๐๐ ๐๐ โข Kuhisi kuungua au maumivu wakati wa kukojoa. โข Miwasho au usumbufu wakati wa kukojoa. โข Kukojoa mara kwa mara hata kama mkojo ni kidogo. โข Kuhisi kubanwa na mkojo muda mfupi baada ya kukojoa. โข Maumivu ya chini ya tumbo au sehemu ya nyonga. โข Mkojo wenye harufu kali au usio wa kawaida. โข Mkojo wenye ukungu au wenye damu wakati mwingine. โข Homa, kutetemeka au maumivu ya mgongo ikiwa maambukizi yameenea hadi kwenye figo. ๐น ๐ก๐๐ก๐ ๐๐๐ก๐๐ช๐๐ญ๐ ๐๐จ๐ฆ๐๐๐๐๐๐ฆ๐๐ ๐จ๐ง๐ ๐๐จ๐๐๐ฅ๐จ๐๐๐? โข Kutokamilisha dozi ya dawa ulizopewa. โข Kutokunywa maji ya kutosha. โข Kushikilia mkojo kwa muda mrefu. โข Kutofanya usafi wa sehemu za siri ipasavyo. โข Magonjwa kama kisukari ambayo huongeza hatari ya maambukizi. โข Kujamiiana kunaweza kuongeza hatari ya UTI kwa baadhi ya wanawake. ๐น ๐๐ช๐ ๐ก๐๐ก๐ ๐ก๐ ๐ ๐จ๐๐๐ ๐จ ๐๐จ๐ฃ๐๐ง๐ ๐ ๐๐ง๐๐๐๐๐จ ๐ ๐๐ฃ๐๐ ๐? Ukipuuzia dalili za UTI, maambukizi yanaweza kuenea hadi kwenye figo na kusababisha matatizo makubwa zaidi. Ndiyo maana ni muhimu kufanyiwa uchunguzi ili kubaini chanzo cha tatizo na kupata matibabu yanayofaa badala ya kutumia dawa bila ushauri wa mtaalamu wa afya. Usipuuzie dalili hizi. Kadri unavyowahi kupata uchunguzi na matibabu, ndivyo unavyoongeza nafasi ya kupona na kupunguza hatari ya maambukizi kujirudia. Afya yako ni mtaji wako nicheki mapema tuone ni namna ipi nzuri tunaweza kukushauri na kukuhudumia tafadhali #fypใท #videoviral #search #milionviews #viral